in , ,

GHADHABU YA RAIS: Wabunge Waasi Wa Jubilee Kuadhibiwa Vikali Baada Ya Kukosa Kufika Kwenye Ikulu Kuhudhuria Mkutano

Rais Uhuru Kentatta ameonya kuwaadhibu wabunge waasi wa Jubilee waliokosa kuhudhuria mkutano wa ikulu leo Jumanne, Februari 13
Rais Uhuru Kentatta ameonya kuwaadhibu wabunge waasi wa Jubilee waliokosa kuhudhuria mkutano wa ikulu leo Jumanne, Februari 13

Rais Uhuru Kenyatta ameonya kuwaadhibu wabunge waasi wa chama cha Jubilee waliokosa kufika Ikulu kwa mkutano wa chama hicho

-Mkutano huo uliongozwa na rais kujadili maswala muhimu ndani ya chama hicho huku bunge la kitaifa likirejelea vikao vyake hivi leo baada ya likizo ndefu ya miezi miwili

-Miongoni mwa maswala makuu kwenye mkutano huo ni pamoja na kupitisha mawaziri wote waliopendekezwa na Rais Uhuru Kenyatta.

Rais Uhuru Kenyatta ameonya kuchukua hatua kali dhidi ya wabunge waasi wa chama cha Jubilee waliokosa kufika kwenye ikulu kwa mkutano wa chama hicho ambao uliandaliwa hivi leo Jumanne, Februari 13.

HABARI NYINGINE:MAKURUTU WAPYA: Zoezi la Kuwasajili Makurutu Wapya Kwenye  Idara ya Jeshi Limeng`oa Nanga

Mkutaono huo ambao uliongozwa na rais Kenyatta ulilengwa kuyapa kipau mbele maswala muhimu ya chama cha Jubilee huku bunge la kitaifa likirejelea vikao vyake hivi leo baada ya likizo ndefu ya miezi miwili. Miongoni mwa maswala makuu yaliyojadiliwa ni pamoja na swala la kupitishwa kwa mawaziri wote pamoja na maafisa wengine waliopendekezwa na rais Kenyatta.

Rais sasa amewarai wabunge wa Jubilee kuhakikisha kwamba mawaziri wote aliowapendekeza yeye wamepitishwa. Pia wameangazia swala la awikilishi wa wanachama wa Jubilee katika kamati muhimu za bunge kama vile tume ya huduma kwa bunge.

Kulingana na ripoti zetu za hapo awali, kuna uwezekano mkubwa kwa ripoti ya kamati ya uteuzi ya bunge kuhusu watu 9 waliopendekezwa kuwa mawaziri kupitishwa, ikizingatiwa idadi kubwa ya wanachama wa Jubilee bungeni.

Zoezi la kuwapiga msasa watu 9 waliopendekezwa kuwa mawaziri na rais Uhuru halikuhudhuriwa na wabunge wa upinzani.

Hatua hii imehiri huku mapambano ya kisiasa yakishamiri baina ya serikali ya jubilee na viongozi wa upinzani. Hapo awali, viongozi wa upinzani walihoji kwamba, hawatukua wakishiriki vikao vya bunge kwa vile hawatambui uhalali wa rais Uhuru Kenyatta.

PIA SOMA:HABARI ZA HIVI PUNDE: Mawakili Wafutilia Mbali Mgomo Wao, Wanihitaji Muda Zaidi Kijiandaa

Ripoti ya kamati ya uteuzi ya Bunge inayohusu watu 9 waliopendekezwa na rais Uhuru kuwa mawaziri inawasilishwa bungeni hivi leo ambako inatarajiwa kujadiliwa na wabunge

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Loading…

Drop a Comment Below

Written by RASHID EMI

RASHID EMI (+254 763 789 784) ni Mtangazaji na Mwandishi wa habari kutoka KENYA na huripoti matukio yote ya ndani na nje ya KENYA kila siku kupitia KDRTV.COM, TWITTER, FACEBOOK, INSTAGRAM na kwenye YOU TUBE.
Mbali na hayo, RASHID EMI. ni Mwigizaji na hupenda kukuza usanii.

Babu Owino has accused president Uhuru of interfering with the high court`s decision against the election petition challenging his victory in August 8 polls

LATEST: Uhuru and Ruto Want Me Out of Parliament – Babu Owino

Uteuzi wa waziri wa michezo na Utamaduni Rashid Mohammed Achesa ilipingwa vikali na baadhi ya wabunge wakitilia shaka kiwango chake cha elimu

Jubilee MPs Turn Wild on Uhuru, They Dispute Nomination of Sports CS Rashid Mohammed Achesa