in

Ukosefu wa vitambulisho watatiza usajili wa wafungwa


Na Sophia Chinyezi
Ukosefu wa vitambulisho miongoni mwa wafungwa ni mojawapo ya changamoto zinazokumba shughuli ya kuwasajili kuwa wapigakura. Shughuli hiyo imetatizwa katika Gereza la King’ong’o, Nyeri kwa kuwa wengi wao hawana stakabadhi hiyo muhimu. Afisa wa IEBC, Nyeri Michael Muchangi amesema ni wanawake wanane pekee ndio wamesajiliwa, ikizingatiwa kwamba waliolengwa ni wafungwa mia tatu.

Ukosefu wa vitambulisho aidha umeshuhudiwa katika Gereza la Vihiga. Afisa Mkuu wa IEBC eneo hilo, Benson Esuza amesema zaidi ya wafungwa kumi na wanne walituma maombi ya kupewa vitambulisho vya kitaifa na vinatarajiwa kutolewa mwishoni mwa wiki hii. Jumla ya wafungwa ishirini na wanne wanatarajiwa kusajiliwa katika shughuli hiyo iliyong’oa nanga jana katika magereza yote nchini.

Kwingineko, wafungwa katika Gereza la Kakamega wamekiandikia barua Chama cha Wanasheria, LSK eneo la Magharibi wakipendekeza kusitishwa kwa usajili magerezani wakilalamikia kutohamasishwa kuhusu shughuli hiyo, mbali na kutaka kuruhusiwa kuwapigia kura viongozi wengine badala la wadhifa wa urais pekee. Aidha wanapendekeza kwamba wanasiasa waruhusiwe kuendesha kampeni hadi magerezani.

Voter apathy hits prisons as inmates fail to register

Ex-IEBC man admits clearing MP facing forgery charges