in ,

MAKALA YA SIKU YA WAPENDANAO: Wakazi Wa Lamu Wapuuzilia Mbali Sherehe Za Siku Ya Wapendanao (Valentines Day)

Wakazi wa Lamu wamepuzilia mbali sherehe za siku ya wapendanao wakihoja kwamba wao wanapendana kila siku
Wakazi wa Lamu wamepuzilia mbali sherehe za siku ya wapendanao wakihoja kwamba wao wanapendana kila siku

-Wakazi wa Lamu wamepuzilia mbali sherehe za siku ya wapendanao wakihoja kwamba wao wanapendana kila siku

-Wameeleza kwamba hawaoni sababu za kutumia rangi nyekundu siku ya wapendanao huku wakieleza kwamba rangi nyekundu huwa huashiria hali ya hatari

Huku siku ya wapendanao ikiadhimishwa kote ulimwenguni, baadhi ya wakazi wa Lamu wameeleza hisia zao kuhusu hatua yao ya kutosherehekea siku hiyo kama wengine. Wamesema kwamba wao wanapendana kila siku na hawaoini sababu ya kutenga siku moja tu ya mapenzi.

le MAKALA YA SIKU YA WAPENDANAO: Wakazi Wa Lamu Wapuuzilia Mbali Sherehe Za Siku Ya Wapendanao (Valentines Day)
Wakazi wa Lamu wadinda kusheherekea siku ya wapendanao, wanasema wao wanapendana kila siku

Japo wamekariri kwamba mapenzi ni mazuri, wamefichua kwamba mapenzi katika mahusiano mbali mbali yanafaa kukuzwa kila siku wala sio siku moja pekee.

Wamesema kwamba kulingana na itikadi yao ya Kiislamu, hukana yeyote ambaye anaruhusiwa kusheherekea siku hiyo maanake itikadi yao inawataka wapendane kila siku wala sio siku ya wapendanao tu.

Vile vile, wameeleza kutounga mkono kuambatanisha rangi nyekundu na mapenzi huku wakisaili kwamba rangi nyekundu kawaida huashiria hali ya hatari.

Huku ulimwegu ukiadhimisha siku kuu ya wapendanao, waumini wa dini la kikatoliki mjini Mombasa wameminika kanisani wakiadhimisha Jumatano ya majevu ambayo inadhimishwa kote duniani huku ikiashiria mwanzo ramsi ya siku 40 za mfungo miongoni mwa waumini wa kanisa la Katoliki.

Kulingana na taarifa tulizopata kutoka Lamu kupitia kwa mwanahabari wetu Mijoge Junior ambaye alikuwa maeneo yale, hakukua na pahala popote panapouzwa maua wala hakukua na watu waliovaa mavazi meupe kuashiria siku ya wapendanao.

Je, wewe ulisherehekea vipi siku ya wapendanao? Ratiba yako ya siku hii ilikuwa vipi? Tupe hadithi yako.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Loading…

Drop a Comment Below

Written by RASHID EMI

RASHID EMI (+254 763 789 784) ni Mtangazaji na Mwandishi wa habari kutoka KENYA na huripoti matukio yote ya ndani na nje ya KENYA kila siku kupitia KDRTV.COM, TWITTER, FACEBOOK, INSTAGRAM na kwenye YOU TUBE.
Mbali na hayo, RASHID EMI. ni Mwigizaji na hupenda kukuza usanii.

Mudavadi to Punish ANC MPs for Criticizing him For Skipping Odinga’s Oath-taking Ceremony

Aliyekuwa seneta wa Machakos Johnson Muthama amehapa kugonga Kalonzo Musyoka kwa bibilia iwapo hataapishwa

Nitagonga Kichwa Chake Kalonzo Kwa Bibilia Iwapo Hataapishwa- Johnson Muthama