in , ,

Raila Kuanza Kufanya Kazi Kama Rais, Ako Tayari Kumenyana Na Jubilee

Raila Odinga amekiri kuanza rasmi kufanya kazi kama rais na hatishwi kutiwa nguvuni na utawala wa Jubilee
Raila Odinga amekiri kuanza rasmi kufanya kazi kama rais na hatishwi kutiwa nguvuni na utawala wa Jubilee

Raila Odinga amekiri kuanza rasmi kufanya kazi kama rais na hatishwi kutiwa nguvuni na utawala wa Jubilee

-Odinga ashtumu serikali kwa kuhitilafiana na idara ya mahakama na vile vile kupuuza maagizo ya mahakama. Pia amelaumu serikali kwa kutumia idara ya polisi kuwangaisha viongozi wa upinzani

-Raila aliongea hayo katika mazishi kule Ebusakami katika ngome ya siasa ya Mudavadi ambaye hakuhudhuria mazishi hayo

Kiongozi wa Muungano wa NASA Raila Odinga amesema kwamba ataanza kufanya kazi kama rais wa watu na hatishwi na lolote.

HABARI NYINGINE:George Kinoti na Joseph Boinett Warushia Mzigo Idara Ya Uhamiaji Kuhusu Kufurushwa Kwa Miguna Miguna

Raila Odinga alikuwa akiongea hayo katika hafla mazishi ya babake mkurungenzi wa mawasiliano wa chama cha ODM Philip Etale kule Embusakami jimbo la Vihiga.

Raila alistumu serikali ya Jubilee kwa kuingilia majukumu ya idara ya Mahakama na hata kupuuza maagizo ya mahakama. Vile vile amelaumu serikali ya jubilee kwa kutumia idara ya polisi kuwahangaisha viongozi wa upinzani

Viongozi wengine waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Amos Wako ambaye alitetea Raila Odinga dhidi ya kushtakiwa na kosa la uhaini kufutia kuapishwa kwake.

Hata hivyo, kiongozi wa chama cha ANC Musalia Mudavadi hakuhudhuria hafla hiyo iliyofanyika katika ngome yake ya kisiasa. Swala hili lilitia hofu wafuasi wengi wa muungano wa NASA huku wakihofia ushirikiano miongoni mwa vigogo wa muungano huo wa NASA.

Ikumbukwe kwamba Muasilia Mudavadi, Kalonzo Musyoka na Moses Wetangula vile vile hawakudhuria hafla ya kuapishwa kwa Raila Odinga, jambo ambalo lilipokelewa na hisia mbali mbali miongoni mwa wafausi wa NASA huku wengine wakihoji kwamba, vinara hao watatu walisaliti bwana Odinga. Hata hivyo, Raila aliwahakikishia wafuasi wa NASA kwamba muungano huo uko imara na utaendelea kushirikiana kwa vyovyote vile.

Hapo awali, Ralia katika mahojiano na shirika la utangazi la kimataifa la BBC alidokeza kwamba anataka uchaguzi uandaliwe upya kufikia mwezi wa Agosti mwakani.

PIA SOMA:KUMEHARIBIKA: MOSES KURIA ANATAKA VIONGOZI ZAIDI WA UPINZANZI KUFURUSHWA!

Hi imejiri siku chache tu baada ya serikali ya Jubilee kutangaza msako mkali dhidi ya viongozi wa upinzani haswa, wale waliohusika katika kuanda hafla ya kuapishwa kwake Raila.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Loading…

Drop a Comment Below

Written by RASHID EMI

RASHID EMI (+254 763 789 784) ni Mtangazaji na Mwandishi wa habari kutoka KENYA na huripoti matukio yote ya ndani na nje ya KENYA kila siku kupitia KDRTV.COM, TWITTER, FACEBOOK, INSTAGRAM na kwenye YOU TUBE.
Mbali na hayo, RASHID EMI. ni Mwigizaji na hupenda kukuza usanii.

Interior CS Matiang’i Suffers Setback after Court Stops Gazette Notice Outlawing NRM

NASA Chief Raila Odinga Accuses Jubilee Government of Violating the  Constitution and Human Rights