in , ,

NAJUA UHURU ANANIANDAMA LAKINI NIKO TAYARI KUKABILIANA NAYE- RAILA ODINGA

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga ameshtumu serikali kwa kukandamiza viongozi wa muungano wa upinzani NASA ilhali inamwinda yeye
Kiongozi wa upinzani Raila Odinga ameshtumu serikali kwa kukandamiza viongozi wa muungano wa upinzani NASA ilhali inamwinda yeye

-Kiongozi wa upinzani Raila Odinga ameshtumu serikali kwa kukandamiza viongozi wa muungano wa upinzani NASA ilhali inamwinda yeye

-Raila alizungumza haya katika mahojiano na runinga ya KTN huku akikiri kuwa yu tayari kukabiliana na hali yoyote katika hari yake ya kuleta mageuzi ya kichaguzi

-Pia akizungumza kuhusu swala la Miguna Miguna, Raila ilisisitiza kwamba vuguvugu la NRM iliyoharamishwa baado itaendelea kutekeleza shuguli zake

-Kiongozi huyo wa muungano wa NASA Raila Odinga akiri kwamba ako tayari kulipa gharama yoyote kama hivyo ndivyo itamaanisha kuafikiwa kwa mageuzi ya kichaguzi

Raila kwenye mahojiano na runinga ya KTN, alishtaki serikali kwa kuwatia nguvu na kukandamiza baadhi ya viongozi wa upinzani huku anayewindwa kwa uhalisi ni yeye

HABARI NYINGINE:KUMEHARIBIKA: MOSES KURIA ANATAKA VIONGOZI ZAIDI WA UPINZANZI KUFURUSHWA!

Raila Odinga aliongeza kwamba, atazidi kupigania mageuzi ya kichaguzi bila kujali alichotaja kama mbinu ya ukandamizaji kutoka kwa serikali.

“Nafahamu wanalenga waliokuwepo siku ya hafla ya uapisho. Lakini siwaogopi. Niko tayari kulipa gharama,” alisema Raila jinsi alivyonukuliwa na Standard

Kuhusu swala la jenerali wa kujitwika wa vuguvugu la NRM Miguna Miguna, Raila alisema kwamba hajali na shuguli za vuguvugu hilo litaenedelea kama kawaida.

“Kufurushwa kwake haitaathiri mipango ya vuguvugu la National Resistance Movment (NRM). Kila badiliko lapata kiongozi lake kutoka kwa wananchi na mtu mwingine ataibuka kujaza nafasi ya Miguna,” alieleza Raila Odinga

Katika mahojiano mengine na shirika la habari la kimataifa la BBC hapo awali, kiongozi huyo wa NASA alionyesha ari yake ya kutaka uchaguzi kuandaliwa upya kufikia mwezi wa Agosti mwaka huu.

Hoja ya Raila Odinga imejiri siku chache baada ya serikali ya Jubilee kufanya msururu wa msako mkali dhidi ya viongozi na wandani wa upinzani.

PIA SOMA:Idadi ya Wabunge Ipunguzwe na Wadhifa wa Wakilishi Wanawake Bungeni Ifutiliwe Mbali- Ekuru Aukot

Baadhi ya viongozi wa upinzani walipokonywa magari yao na hata vyeti vyao vya usafiri kubatilishwa. Serikali pia imeweza kukiuka maagizo ya idara ya mahakama mara kadha ili kufanikisha makabiliano yao dhidi ya vingozi wa upinzani.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Loading…

Drop a Comment Below

Written by RASHID EMI

RASHID EMI (+254 763 789 784) ni Mtangazaji na Mwandishi wa habari kutoka KENYA na huripoti matukio yote ya ndani na nje ya KENYA kila siku kupitia KDRTV.COM, TWITTER, FACEBOOK, INSTAGRAM na kwenye YOU TUBE.
Mbali na hayo, RASHID EMI. ni Mwigizaji na hupenda kukuza usanii.

All is Well With Wavinya Ndeti Despite Losing to Mutua.

Mwanamke Mwingereza alipatana na kifo chake alipoelekea kuogelea katika kidimbwi cha maji cha Nairobi Safari Club

HUZUNI: Mwanamke Raia Wa Uingereza Afariki Maji Nairobi Safari Club Akiogelea