in

NASA yasisitiza iko tayari kwa uchaguzi


Na Sophia Chinyezi
“Tuko tayari kushirikiana na IEBC iwapo itawashirikisha washikadau wote katika kufanikisha uchaguzi huru na wa haki.” Ni matamshi yaliyotolewa na mmoja wa vinara wa Muungano wa NASA, Raila Odinga mapema leo wakati wa kikao na wanahabari katika mako makuu ya muungano huo eneo la Capitol Hill, Nairobi.

Raila amesema makosa yaliyoshuhudiwa wakati wa kuwasajili wapiga-kura ambapo watu kadhaa waligunduliwa kuwa na nambari sawa za vitambulisho, yanafaa kushughulikia kwa haraka ili kuzuia wizi wa kura wakati uchaguzi.
Wakati uo huo, amerejelea kauli yake kwamba sajili ya wapigakura inastahili kufanyiwa ukaguzi wa kina na kampuni ambayo ina tajriba ya kutosha katika masuala hayo.

Kwa upande wake kinara mwenza Musalia Mudavadi amesema wasingependa kufanyika kwa uchaguzi usioaminika, hivyo kuitaka IEBC kujitokeza wazi na kujibu masuala waliyoibua, ambayo kufikia sasa hayajajibiwa.

 

Lapsset receives more money to guarantee success

NASA’s checklist for IEBC poll readiness