in ,

HUZUNI: Mwanamke Raia Wa Uingereza Afariki Maji Nairobi Safari Club Akiogelea

Mwanamke Mwingereza alipatana na kifo chake alipoelekea kuogelea katika kidimbwi cha maji cha Nairobi Safari Club
Mwanamke Mwingereza alipatana na kifo chake alipoelekea kuogelea katika kidimbwi cha maji cha Nairobi Safari Club

-Mwanamke Mwingereza alipatana na kifo chake alipoelekea kuogelea katika kidimbwi cha maji cha Nairobi Safari Club

-Rose Mumbi Tidey alidhibitishwa kufa alipowasili katika hospitali ya Bliss Medical Center kufuatia tukio hilo la jioni ya Alhamisi, Februari 8.

-Aliandamana na binti yake mwenye umri wa miaka 5 aliyepiga mayowe alipotazama mamake akizama

Mwanamke raia wa Uingereza lakini mzaliwa wa Kenya, alizama majini na kufa katika kidimbwi cha maji cha Nairobi Safari Club mnamo Ijuma, Februari 8 majira ya jioni.

PIA SOMA:NAJUA UHURU ANANIANDAMA LAKINI NIKO TAYARI KUKABILIANA NAYE- RAILA ODINGA

Rose Mumbi Tidey mwenye umri wa miaka 41, alienda kuogelea majira ya saa tisa jioni kwenye klabu ya Nairobi Safari Club akiwa ameandamana na binti yake Chritine Tidey mwenye umri wa miaka 5

Bintyiye alipiga mayowe wakati alipotazama mama yake akizama majini, ndipo wahudumu wa klabu hiyo walipomtoa majini. Walimpa huduma za kwanza kabla ya kumpeleka hadi kwa hospitali ya Bliss Medical Centre alipodhibitishwa kufa tayari

Kulingana na anyehusika na ulinzi katika klabu hiyo afisa Marcus Opiyo, mwendazake alikuwa katika likizo na aliwasili humo mnamo saa kumi na mbili asubuhi.

PIA SOMA:KUMEHARIBIKA: MOSES KURIA ANATAKA VIONGOZI ZAIDI WA UPINZANZI KUFURUSHWA!

Mwili wake ulipelekwa katika hifadhi ya maiti ya Chiromo huku ukitegea kufanyiwa uchunguzi. Maafisa wa polisi kutoka kituo cha polisi cha Central walikwishaanza uchunguzi kuhusiana na kifo chake Mumbi.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Loading…

Drop a Comment Below

Written by RASHID EMI

RASHID EMI (+254 763 789 784) ni Mtangazaji na Mwandishi wa habari kutoka KENYA na huripoti matukio yote ya ndani na nje ya KENYA kila siku kupitia KDRTV.COM, TWITTER, FACEBOOK, INSTAGRAM na kwenye YOU TUBE.
Mbali na hayo, RASHID EMI. ni Mwigizaji na hupenda kukuza usanii.

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga ameshtumu serikali kwa kukandamiza viongozi wa muungano wa upinzani NASA ilhali inamwinda yeye

NAJUA UHURU ANANIANDAMA LAKINI NIKO TAYARI KUKABILIANA NAYE- RAILA ODINGA

Crackdown on NASA Affiliates Still on. Boinnet Warns Law Breakers; Denying Violating Constitution