in , ,

MIKWARUZANO MIKALI BUNGENI: Mjadala Mkali Unatarajiwa Bungeni Ripoti Ya Tume Ya Uteuzi Ya Bunge Ikijadiliwa

Mjadala mkali unatarajiwa bungeni leo alasiri huku ripoti ya kamati ya uteuzi ya bunge kuhusu watu 9 waliopendekezwa kuwa mawaziri ikijadiliwa
Mjadala mkali unatarajiwa bungeni leo alasiri huku ripoti ya kamati ya uteuzi ya bunge kuhusu watu 9 waliopendekezwa kuwa mawaziri ikijadiliwa

-Mjadala mkali unatarajiwa bungeni leo alasiri huku ripoti ya kamati ya uteuzi ya bunge kuhusu watu 9 waliopendekezwa kuwa mawaziri ikijadiliwa

-Haijabainika kama wabunge wa upinzani watahudhuria kikao cha bunge hivi leo kujadili ripoti hiyo ya kamati ya uteuzi ya bunge

-Hapo jana, Rais Kenyatta aliongoza mkutano wa chama cha Jubilee huku akirai wabunge hao kuhakikisha kwamba ripoti hiyo kuhusu waliopendekezwa kuhudumu katika baraza la mawaziri limepitishwa

Mjadala mkali unatarajiwa hivi leo Jumatano, Februari 14 katika bunge la kitaifa wakati wabunge hao watakaokuwa wakijadili ripoti ya kamati ya uteuzi ya bunge kuhusu majina tisa ya waliopendekezwa na rais Uhuru Kenyatta kuhudumu katika baraza la mawaziri.

HABARI NYINGINE:GHADHABU YA RAIS: Wabunge Waasi Wa Jubilee Kuadhibiwa Vikali Baada Ya Kukosa Kufika Kwenye Ikulu Kuhudhuria Mkutano

Hata hivyo, huenda wabunge wa upinzani wakasusia kikao hicho cha bunge kitakachozalisha mjadala mkali jinsi walivyosusia zoezi la kuwapiga msasa watu tisa waliopendekezwa kuwa mawaziri.

Kulingana na ripoti ambazo zimefikia KDRTV.com, wabunge wa upinzani wamesema kwamba, watususia kikoa hicho cha bunge ambacho kitang`oa nanga alasiri ya leo.

Hapo jana Jumanne, Februari 13, rais Uhuru Kenyatta aliongoza mkutano wa wabunge wa chama cha Jubilee huku maswala makuu yaliyojadiliwa ni pamoja na wabunge wa Jubilee kuhakikisha kwamba, bunge limepitisha majina yote tisa ya watu waliopendekezwa na rais kuhudumu katika baraza la mawaziri.

Bunge la kitaifa lilirejelea vikao vyake hapo jana huku mikwaruzano mikali ikishuhudiwa baina ya wabunge wa serikali na wabunge wa upinzanzi kuhusu swala la wabunge wa upinzani kupokonywa walizi wao.

PIA SOMA:MAKURUTU WAPYA: Zoezi la Kuwasajili Makurutu Wapya Kwenye  Idara ya Jeshi Limeng`oa Nanga

Watakaojadiliwa bungeni hivi leo kuhusu ubora wao kuhusiana na nyadhifa mbali mbali kwenye baraza la mawaziri ni pamoja na aliyekuwa msimamizi katika kampuni ya Royal Media Services Bi. Farida Karoney, Mohammed Achesa, John Munyes na Ukur Yattani miongoni mwa wengine

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Loading…

Drop a Comment Below

Written by RASHID EMI

RASHID EMI ni Mtangazaji na Mwandishi wa habari kutoka KENYA na huripoti matukio yote ya ndani na nje ya KENYA kila siku kupitia KDRTV.COM, TWITTER, FACEBOOK, INSTAGRAM na kwenye YOU TUBE.
Mbali na hayo, MIJOGE JR. ni Mwigizaji na hupenda kukuza usanii.

POLICE BOSSES STRIKE AGAIN: Boinnet and Kinoti Excuse Themselves From Attending their Case Explaining Miguna’s Saga

Mudavadi to Punish ANC MPs for Criticizing him For Skipping Odinga’s Oath-taking Ceremony