in , ,

HABARI ZA HIVI PUNDE: Mawakili Wafutilia Mbali Mgomo Wao, Wanihitaji Muda Zaidi Kijiandaa

Mawakili nchini Kenya kupitia chama cha wanasheria nchini LSK wameahairisha mgomo wao kutenga muda Zaidi kwa maandalizi thabiti
Mawakili nchini Kenya kupitia chama cha wanasheria nchini LSK wameahairisha mgomo wao kutenga muda Zaidi kwa maandalizi thabiti

-Mawakili nchini Kenya kupitia chama cha wanasheria nchini LSK wameahairisha mgomo wao kutenga muda Zaidi kwa maandalizi thabiti

-Wamesitisha mpango wao wa kususia mahakama kujianda vilvyo kugoma dhidi ya serikali kuu ya Jubilee

-Mgomo huo ulipangwa kung`oa nanga hivi leo Jumatatu, Februari 12 na ingedumu kwa muda wa siku tano

Chama cha wanasheria nchini LSK kwa habari yao kwa wanahabari, wametamgaza kusitisha mgomo wao kwa muda ili kutenga nafasi zaidi ya mashauriano kuhusu maandano ambayo yalifaa kung`oa nanga hivi leo Jumatatu, Febrauri 12.

HABARI NYINGINE:Jaji David Maraga ni Kibaraka Cha NASA- Viongozi wa Milma Kenya

Kupitia kwa habari za KDRTV.com hapo jana, mawakili nchini walipanga kuandaa mgomo ili kalalamikia jambo walilorejelea kama mazoea ya serikali kuu kukaidi agizo la mahakama na vile vile kuidharau idara ya mahakama.

Pia, walishtumu serikali kuu kukiuka haki za waliozuiliwa korokoroni na kutumia idara ya polisi visivyo kukandamiza wanchi wa Kenya bila sababu dhabiti.DVw0gTqW4AEc5uh HABARI ZA HIVI PUNDE: Mawakili Wafutilia Mbali Mgomo Wao, Wanihitaji Muda Zaidi Kijiandaa

Kupitia kwa taarifa ya LSK kwa vyombo vya habari, wamehoji kwamba, wamechukua hatua ya kisitisha mgomo huo kwa muda ili kutenga nafasi ya mashauriano  zaidi.

Mgomo huo ulipania kuathiri mahakama yote isipokuwa yale yanayoshugulikia kesi za uchaguzi. Mawakili wangevaa kanda za manjano wakati wa mgomo huo kuonyesha shutuma zao kwa serikali kuu kukaidi maagizo ya mahakama.

Hatua hii ya mawakili yamejiri siku chache baada ya serikali kuu kupitia kwa mamlaka ya mawasiliano nchini kuzima mitambo ya runinga za Citizen, KTN, NTV na Inooro kufutia hafla ya kuapishwa kwa Raila Odinda. Mahakama baadaye iliamuru mitambo hiyo ifunguliwe lakini serikali ikakaidi agizo hilo.

PIA SOMA:Wahudumu Katika Sekta ya Usafiri Kiambu Wanataka Charity Ngilu Akamatwe Kwa Kuamuru Magari Yachomwe

Tukio la pili ni pale jenerali wa vuguvugu la NRM Miguna Miguna alikamatwa na kusafirishwa nchini Canada kinyume cha sheria. Hapo awali, mahakama kuu kupitia kwa jaji Luka Kimari iliagiza Miguna Miguna kuachiliwa huru na baadala yake kupewa dhamana. Agizo hilo pia lilikiukwa. Isitoshe, mahakama pia iliamuru wakuu wa idara ya polisi kufika mahakamani wakiwa wameandamana na Miguna Miguna lakini hilo pia likakiukwa na serikali.

Swala hilo lilivutia hisia za jaji mkuu David Maraga ambaye pia alilaumu serikali kwa kadharau idara hiyo ya mahakama.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Loading…

Drop a Comment Below

Written by RASHID EMI

RASHID EMI ni Mtangazaji na Mwandishi wa habari kutoka KENYA na huripoti matukio yote ya ndani na nje ya KENYA kila siku kupitia KDRTV.COM, TWITTER, FACEBOOK, INSTAGRAM na kwenye YOU TUBE.
Mbali na hayo, MIJOGE JR. ni Mwigizaji na hupenda kukuza usanii.

Human Rights Activist Haron Ndubi Arrested

Polisi mnamo Jumapili, Februari 11 usiku walimtia nguvu wakili Harun Ndubi kwa kuendesha gari akiwa mlevi

MAKUBWA: WAKILI WA MIGUNA MIGUNA AKAMATWA NA POLISI NAIROBI!