in , ,

Mawakili Kuanda Mgomo wa Kitaifa, Wanasuta  Serikali Kudharau Idara Ya Mahakama

Mawakili kupitia Chama cha Wanasheria Nchini (LSK) wametangaza kuanda mgomo kuanzia Jumatatu, Februari 12 kulalamikia mazoea ya serikali kukiuka maagizo ya mahakama
Mawakili kupitia Chama cha Wanasheria Nchini (LSK) wametangaza kuanda mgomo kuanzia Jumatatu, Februari 12 kulalamikia mazoea ya serikali kukiuka maagizo ya mahakama

-Mawakili kupitia Chama cha Wanasheria Nchini (LSK) wametangaza kuanda mgomo kuanzia Jumatatu, Februari 12 kulalamikia mazoea ya serikali kukiuka maagizo ya mahakama

-Wamelaumu serikali kwa kukiuka haki za waliozuiliwa korokoroni na vile vile kutumia polisi kuhangaisha wakenya bila sababu

-Mgomo huo wa kitaifa utadumu kwa muda wa siku tano huku mahakama zinazoshugulikia kesi za uchaguzi zikiendelea kuhudumu.

Mawakili kupitia Chama Cha Wanasheria Nchini (LSK) wametangaza kuanda mgomo wa kitaifa hapo kesho Jumatatu, Februari 12 kulalamikia mazoea ya serikali kuu kukaidi agizo la mahakama na kutumia idara ya polisi kinyume cha sheria. Wamesema shuguli za mahakama zitakwama watakaposusia mahakama kwa muda ya siku tano.

HABARI NYINGINE:Watu 9 Waliopendekezwa Kuwa Mawaziri Kujua Hatima Yao Jumatano Lijalo, Rafael Tuju Hatahojiwa

“Wanachama wetu wote watasusia mahakama kwa siku tano kuanzia Jumatatu (kesho) kupinga tabia ya serikali, na maafisa wake wakuu kutoheshimu amri za mahakama,” alisema mwenyekiti wa chama cha LSK wakili Isaac Okero kwenye taarifa kwa wanahabari.

Okero alisisitisha kwamba ni wajibu wa kila mtu kuheshimu sheria. Alisema serikali haiwezi kudharau sheria na itarajie wanchi keheshimu hizo hizo sheria. Kulingana na Okero, nchi ambayo haishemu sheria na katiba hutumbukia katika machafuko.

Kulingana na LSK, mawakili watavaa nguo zao rasmi na kufunga kanda za manjano kuashiria wanagoma katika miji mbali mbali humu nchini.

Kwa upande mwingine, mahakama zinazoshugulikia kesi za uchaguzi zitaendelea kuhudumu kwa kile LSK ilisema kwamba ni makataa yaliyowekewa kesi hizo.

Tangazo hilo la LSK limejiri siku chache baada ya Jaji mkuu David Maraga kufichua hofu yake kuhusiana na hatua ya serikali kuu kukiuka maagizo ya mahakama.

Chini ya muda wa wiki moja uliopita, serikali kuu imekuwa ikipuuza maagizo muhimu ya idara ya mahakama, swala ambalo lilikashifiwa na mashirika mbali mbali na hata viongozi wa kidini pamoja na raia.

Mawakili pia wamelaumu serikali kuu kwa kutumia polisi kukiuka haki za waliozuiliwa korokoroni na vile vile kuhangaisha wananchi bila sababu ya kutosha

Katika tukio la kwanza, serikali ilikaidi agizo la mahakama lililoamuru mamlaka ya mawasiliano nchini kufungua mitambo ya runinga za Citizen, KTN, NTV na Inooro baada ya kuzima mnamo Januari 30 kufuatia hafla ya kuapishwa kwake Raila Odinga.

Tukio la pili ni pale idara ya polisi ikiongozwa na inspekta jenerali wa polisi Joseph Boinett kukataa Kuachilia Miguna Miguna huru na kupewa dhamana ya sh50,000. Vile vile Boinett alikaidi agizo la mahakama kufika mahakamani binafsi akiwa ameandamana na Miguna Miguna.

PIA SOMA:HUZUNI NA MAJONZI: Hafla Ya Kuwaaga Wahasiriwa wa Ajali Ya Ndege ya Ziwa Nakuru Ilifanyika Leo

Sasa chama cha wanasheria nchini imefichua kwamba watashtaki wale wote waliohusika katika kukiuka agizo la mahakama ili wakabiliwe na mkondo wa sheria.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Loading…

Drop a Comment Below

Written by RASHID EMI

RASHID EMI (+254 763 789 784) ni Mtangazaji na Mwandishi wa habari kutoka KENYA na huripoti matukio yote ya ndani na nje ya KENYA kila siku kupitia KDRTV.COM, TWITTER, FACEBOOK, INSTAGRAM na kwenye YOU TUBE.
Mbali na hayo, RASHID EMI. ni Mwigizaji na hupenda kukuza usanii.

I’ll Be Back to Kenya Soon. Miguna says Plans Underway to Return to Kenya

Matiang’i Defends Himself Against Condemnation Resulting from Recent Government Crackdown on NASA