in ,

BONGO: Mtoto wa Hamisa Mobetto ni Mjukuu Wangu- Mama Diamond

Mtoto wa Hamisa Mobetto ni Mjukuu Wangu- Mama Diamond Platinumz
Mtoto wa Hamisa Mobetto ni Mjukuu Wangu- Mama Diamond Platinumz

Mama wake mzazi staa wa Bongo fleva Diamond Platinumz almaarufu Bi. Sandra amefunguka na kukiri kwamba mtoto wa Hamisa pia ni mjukuu wake

HABARI NYINGINE:MAAMUZI YA MAHAKAMA: Mahakama Kuadhibu Maafisa Wakuu wa Polisi Kuhusu Kufurushwa kwa Miguna Miguna

Maisha ya staa huyo wa Bongo Fleva yameweza kukumbwa na makovu yanayohusu uhusiano wake wa kifamilia. Mwishoni mwa mwaka jana, Diamond aluzua tukio la mwaka baada ya kukiri kwenye redio kwamba amezaa na Hamisa ambaye pia alisema kwamba amekuwa mpango wake wa kando kwa muda wa miaka tisa na Zaidi

Baada ya sakata hiyo Zari ambaye ndiye mpenzi wake anayemwita bibi, aliwaka moto lakini baadaye Zari alimsamehe baba watoto wake na wakaendelea na mahusiano yao. Hapo ndipo familia ya Diamond ilipokumbatia Zari Zaidi na kumtupilia mbali Hamisa na mtoto wake.

Wakati wote, wengi wamekuwa wakijiuliza mbona familia hiyo ya Diamond haijakuwa na ukaribu na mtoto ya Hamisa Prince Dully kama ilivyofanya kwa watoto wa Zari, Prices Tiffah na Prince Nillan.

Katika wakati wa hivi majuzi, staa huyo wa Bongo fleva tena amegonga vichwa vya habari na hata habari zake kuenea katika mtandao wa kijami kuhusu mahusiano baina yake na mpenzi wake Zari.

Safari hii Zari anaonekana kushindwa kuvumilia sakata za Diamond. Hii ni baada ya Zari kusitisha ufuasi wake wa familia yote ya Diamond kwenye mtandao akiwemo mama wa Diamond Bi. Sandra

Licha ya hayo yote, mama mzazi wake Diamond amekiri kwamba, mtoto wake Hamisa, Price Dully ama Dylan pia ni mjukuu wake.

Habafi hii ilichipuka kutoka kwa mtandao wa Instagram wakati Bi. Sandra alipoposti picha ya mjukuu wake Nillan na shabiki fulani akamuuliza, “uwe unapoti hata Dylan kwani naye si mjukuu wako?”

Huku akirejelea swali hilo, alijibu, “Usijali ntamposti yule ni mjukuu wangu hivyo lazima nimposti tu”

Zari pia ambaye ako na watoto ambao baba yao siye Diamond, amekuwa na wakati mgumu kuweza kukaa kwenye mahusiano hasa ya kifamilia na staa huyo wa bongo fleva Diamond Platinumz, Je ataendelea kuvulia au, ni hatua ipi atakayo chukua Zari kuhusu swala la Diamond kutokuwa na wazo mseto katika uhusiano mmjoa?

 

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Loading…

Drop a Comment Below

Written by RASHID EMI

RASHID EMI (+254 763 789 784) ni Mtangazaji na Mwandishi wa habari kutoka KENYA na huripoti matukio yote ya ndani na nje ya KENYA kila siku kupitia KDRTV.COM, TWITTER, FACEBOOK, INSTAGRAM na kwenye YOU TUBE.
Mbali na hayo, RASHID EMI. ni Mwigizaji na hupenda kukuza usanii.

IG Joseph Boinett and DCI George Kinoti have filed an application not to feature in court in person during the court hearing of the Miguna`s case

MAAMUZI YA MAHAKAMA: Mahakama Kuadhibu Maafisa Wakuu wa Polisi Kuhusu Kufurushwa kwa Miguna Miguna

Idadi ya waliouwawa na polisi kufuatia maandamano ya Kisumu kutetea Miguna Miguna imefikia watu watatu

Idadi ya Wafuasi wa NASA Waliouwawa Na Polisi Katika Maandamano ya Kisumu Yaongezeka