in , ,

MAKURUTU WAPYA: Zoezi la Kuwasajili Makurutu Wapya Kwenye  Idara ya Jeshi Limeng`oa Nanga

Zoezi la kuwasajili makurutu wapya kujiunga na kikosi cha ulinzi cha KDF limeng`oa nanga  hivi leo
Zoezi la kuwasajili makurutu wapya kujiunga na kikosi cha ulinzi cha KDF limeng`oa nanga  hivi leo

-Zoezi la kuwasajili makurutu wapya kujiunga na kikosi cha ulinzi cha KDF limeng`oa nanga  hivi leo

-Zoezi hilo lilianaza leo huku vijana wengi waliojitokeza wakitemwa kulingana na upungufu wa kielimu na maumbile

-Idara ya jeshi sasa inalenga kuwasajili makurutu wapatao 2000 katika zoezi hilo litakalochukua mwezi mmoja

Zoeli la kuwasijili makurutu wapya kwenye idara ya jeshi liling`oa naga hivi leo Jumatatu, Februari 12 huku vijana wengi waliojitokeza wakilalamika kutemwa na ari yao ya kujiunga na kikosi cha ulinzi cha KDF ikizimwa.

HABARI NYINGINE:Jaji David Maraga ni Kibaraka Cha NASA- Viongozi wa Milma Kenya

Kulingana na habari zilizotufikia, baadhi ya vijana wengi waliojitokeza, walitemwa kutokana na upungufu wa kiuzani, kielimu na kimaumbile.

Kule pwani kwa mfano, baadhi ya vijana walitemwa kutokana na uraibu wa mihadarati huku miraa ikichangia pakubwa. Viongozi wa pwani sasa wameshauriwa kushawishi vijana kuacha uraibu wa miraa ambao umeathiri afya yao.

Naibu mkuu wa majeshi luteni jenerali Joseph Kasaon sasa amehahakikishia wananchi kwamba zoezi hilo litakuwa wa huru na haki huku akikiri kwamba zoezi hilo litasimamiwa afisa mkuu wa sajili huku akipewa wasaidizi wengine sita. Watakaoshiriki kuhakiki zoezi hilo ni pamoja na washikadau wengine kama idara ya ujasusi, tume ya maadili na kupambana na ufisadi,shirika la Transparency International miongoni mwa mashirika mengine.

Jeneral Kasaon sasa amerai wakenya kuripoti visa vyovyote vya ufisadi au ukosefu wa nidhamu kuhusiana na zoezi hilo.

Zoezi hilo liling`oa nanga katika sehemu mbali mbali nchini huku kule Limuru vijana waliojitokeza wakitemwa kutokana na rangi ya meno yao.

Vijana waliokosa kuafiki viwango hitajika vya elimu walishauriwa kurudi kupata masomo huku wenye shahada wakiraiwa kungoja kujiunga na kitengo cha wanajeshi wa KADET.

PIA SOMA:HABARI ZA HIVI PUNDE: Mawakili Wafutilia Mbali Mgomo Wao, Wanihitaji Muda Zaidi Kijiandaa

Zoezi hilo linatarajiwa kuendelea hapo kesho katika maeneo mbali mbali nchini.

Zoezi hili limejiri wakati kuna joto jingi la kisiasa huku makabiliano baina ya utawala wa Jubilee na viongozi wa upinzani yakiendelea.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Loading…

Drop a Comment Below

Written by RASHID EMI

RASHID EMI (+254 763 789 784) ni Mtangazaji na Mwandishi wa habari kutoka KENYA na huripoti matukio yote ya ndani na nje ya KENYA kila siku kupitia KDRTV.COM, TWITTER, FACEBOOK, INSTAGRAM na kwenye YOU TUBE.
Mbali na hayo, RASHID EMI. ni Mwigizaji na hupenda kukuza usanii.

EXCLUSIVE: Miguna Miguna Sues the Government for Deportation.

Babu Owino Suffers a Major Blow as Court Orders Vote Recount in Embakasi East Constituency