in , ,

Wahudumu Katika Sekta ya Usafiri Kiambu Wanataka Charity Ngilu Akamatwe Kwa Kuamuru Magari Yachomwe

Wahudumu Katika Sekta ya Usafiri Kiambu Wanataka Charity Ngilu Akamatwe Kwa Kuamuru Magari Yachomwe
Wahudumu Katika Sekta ya Usafiri Kiambu Wanataka Charity Ngilu Akamatwe Kwa Kuamuru Magari Yachomwe

Wahudumu katika sekta ya usafiri Limuru wameandama huku wakitaka Charity Ngilu akamatwe kwa kuamuru vijana wachome magari

-Wahudumu waliojawa na hasira walimshtumu Gavana Ngilu kwa kueneza ukabila baada ya kuamuru vijana kuchoma magari yanayoleta makaa katika kaunti hiyo

-Ngilu alilenga kuzuia biashara ya  makaa ambayo imepelekea ukataji miti kiholela kule Ukambani

Wahudumu katika sekta ya usafiri kule Limuru, kaunti ya Kiambu mnamo Jumamosi, Februari 10 waliandamana wakitaka Gavana wa Kitui Charity Ngilu kukamatwa kwa kushawishi vijana kuchoma malori yanayosafirisha makaa ndani ya kaunti yake

0fgjhs3g10oheiapj.7aacf25a Wahudumu Katika Sekta ya Usafiri Kiambu Wanataka Charity Ngilu Akamatwe Kwa Kuamuru Magari Yachomwe
Wahudumu katika sekta ya usafiri Limuru wameandama huku wakitaka Charity Ngilu akamatwe kwa kuamuru vijana wachome magari

Waandamanaji waliojawa na hasira waliwasha moto kwenye baraste ya Nairobi-Nakuru na kuziba barabara na magogo huku wakishtumu Ngilu kwa kueneza ukabila

HABARI NYINGINE:Watu 9 Waliopendekezwa Kuwa Mawaziri Kujua Hatima Yao Jumatona Lijalo, Rafael Tuju Hatahojiwa

Kulingana na ripoti ambazo zimefikia KDRTV.com, mbunge wa Maeneo ya Kiambu Peter Mwathi na diwani wa Limuru ya kati Joseph Kaheya walimshauri inspekta mkuu wa polisi Joseph Boinett kukamata Ngilu kwa vile kuna ushaidi wa kutosha kudhibitisha kwamba, Ngilu aliamuru vijana kuchoma malori

Mwathi pia alitaka tume ya uwiiano na utangamano kuchunguza tukio la kuchomwa kwa gari huku akiongeza kwamba watashtaki Charity Ngilu kwenye baraza la magavana.

“Tunahitaji magavana wetu kufahamu kwamba tunahitajiana, watu wetu wanafanya biashara kutoka kaunti mbali mbali,” alieleza Mwathi

Kwa upande wake Ngilu, hatua yake huenda ni kujaribu kurekebisha hali mbaya ya mazingira ambayo imechangiwa na ukataji haramu wa miti katika maeneo ya ukambani.

Aliyehusika na lori lilochomwa David Kariuki naye amekana madai ya kununua makaa kutoka kitui kwani Gavana Ngilu alipiga marufuku biashara ya makaa katika kaunti hiyo.

Inasemekana kwamba Ngilu na wasaidizi wake walisimamisha lori hilo na kuuliza leseni ya dereva, cheti cha usafiri, risiti ya kaunti and stakabadhi ya shirika.

Polisi wakiongozwa na kamanda Andiel Nyange, waliingilia kati kutuliza hali na kuwaondoa waandamanaji walioziba kilomita 3 ya barabara ya Kwambira kuelekea Kamandura.

Nyange alihakikishia wakazi hao kwamba waliohusika katika tukio hilo watakabiliwa vilivyo na mkondo wa sheria bila kujali hadhi yao

PIA SOMA:HUZUNI NA MAJONZI: Hafla Ya Kuwaaga Wahasiriwa wa Ajali Ya Ndege ya Ziwa Nakuru Ilifanyika Leo

Pia alikiri kwamba polisi wameanza kumchunguza Charity Ngilu na bila shaka, yeyote ambaye alihusika kwa kuvunja sheria atakabiliwa vilivyo.

0fgjhs2ai1r011dvj.fe69a782 Wahudumu Katika Sekta ya Usafiri Kiambu Wanataka Charity Ngilu Akamatwe Kwa Kuamuru Magari Yachomwe
Wahudumu katika sekta ya usafiri Limuru wameandama huku wakitaka Charity Ngilu akamatwe kwa kuamuru vijana wachome magari

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Loading…

Drop a Comment Below

Written by RASHID EMI

RASHID EMI ni Mtangazaji na Mwandishi wa habari kutoka KENYA na huripoti matukio yote ya ndani na nje ya KENYA kila siku kupitia KDRTV.COM, TWITTER, FACEBOOK, INSTAGRAM na kwenye YOU TUBE.
Mbali na hayo, MIJOGE JR. ni Mwigizaji na hupenda kukuza usanii.

Watu 9 Waliopendekezwa Kuwa Mawaziri Kujua Hatima Yao Jumatona Lijalo, Rafael Tuju Hatahojiwa

Watu 9 Waliopendekezwa Kuwa Mawaziri Kujua Hatima Yao Jumatano Lijalo, Rafael Tuju Hatahojiwa

IG Joseph Boinett and DCI George Kinoti have filed an application not to feature in court in person during the court hearing of the Miguna`s case

MORE FIRE: Jubilee Devising To Arrest Senior NASA Leaders in another Round of Powerful Crackdown