in , ,

George Kinoti na Joseph Boinett Warushia Mzigo Idara Ya Uhamiaji Kuhusu Kufurushwa Kwa Miguna Miguna

Inspekta jenerali wa polisi Joseph Boinett na mkurugenzi wa idara ya upelelezi George Kinoti wamekana madai ya kukiuka agizo la mahakama katika kesi ya Miguna Miguna
Inspekta jenerali wa polisi Joseph Boinett na mkurugenzi wa idara ya upelelezi George Kinoti wamekana madai ya kukiuka agizo la mahakama katika kesi ya Miguna Miguna

-Inspekta jenerali wa polisi Joseph Boinett na mkurugenzi wa idara ya upelelezi George Kinoti wamekana madai ya kukiuka agizo la mahakama katika kesi ya Miguna Miguna

-Kupitia kwa hati kiapo waliowasilisha mahakamani, wawili hao wamelaumu idara ya uhamiaji na kiitaka ieleze sababu haswa ya kufanya Miguna afurushwe

-Idara ya uhamiaji imedokeza kwamba ilipata amri kutoka kwa waziri wa usalama na maswala ya ndani Daktari Fred Matiang`i

Inspekta jenerali wa polisi Joseph Boinett na mkurugenzi wa idara ya upelelezi George Kinoti hii leo wamekana madai ya kudharau na kukiuka agizo la mahakama kuhusu kesi ya wakili Miguna Miguna

PIA SOMA:NAJUA UHURU ANANIANDAMA LAKINI NIKO TAYARI KUKABILIANA NAYE- RAILA ODINGA

Kupitia kwa hati kiapo waliowasilisha kotini hivi leo, maafisa hao wawili baadala yake wameitupia lawama idara ya uhamiaji na kuitaka kueleza ni kwa nini Miguna Miguna alifurushwa nchini.

Awali, jaji wa mahakama kuu Luka Kimaru alitaka hati kiapo kutoka kwa inspekta jenerali wa polisi Boinet, mkurugenzi wa idara ya upelelezi Kinoti na idara ya uhamiaji kuelezea ni kwa nini wasiadhibiwe kwa kukiuka agizo la mahakama.

Baada ya maamuzi hayo ya mahakama, mchezo wa paka na panya imeibuka miongoni mwa Inspekta jenerali wa polisi Joseph Boinett, mkurugenzi wa idara ya upelelezi George Kinoti na idara ya uhamiaji.

Idara ya uhamiaji kupitia kwa mkurugenzi yake Godwin Kihalangwa ilisema kwamba haikujuwa kwamba kulikuwa na agizo kuhusu wakili Miguna Miguna na kuongezea kwamba, idara hiyo ilipata amri kutoka kwa waziri wa usalama na maswala ya ndani Daktari Fred Matiang`i ili kufukuza Miguna. Matiang`i alihoji kwamba Miguna Miguna hakuwa na kibali cha kukaa humu nchini.

Inspekta jenerali wa polisi Joseph Boinett alisema kuwa polisi walimwachilia huru Miguna Miguna kama ilivyoagiza mahakama, lakini baadaye maafisa wa idara ya uhamiaji wakamtia nguvu na kumsafirisha hadi Canada.

HABARI NYINGINE:KUMEHARIBIKA: MOSES KURIA ANATAKA VIONGOZI ZAIDI WA UPINZANZI KUFURUSHWA!

Hata hivyo, Miguna alieleza kwamba yeye ni raia wa Kenya kwa kuzaliwa na hajawi kusaliti au kukana uraia wake wa Kenya. Miguna sasa amekiri kwamba ameanza kushugulikia safari yake ya kurudi Kenya. Aidha, ameitaka mahakama kuwaadhibu waliohusika katika kufurushwa kwake kwani yeye ni mzaliwa wa Kenya na hapaswi kunyanganywa uraia wake pasipo yeye kuwasilisha ombi hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Loading…

Drop a Comment Below

Written by RASHID EMI

RASHID EMI ni Mtangazaji na Mwandishi wa habari kutoka KENYA na huripoti matukio yote ya ndani na nje ya KENYA kila siku kupitia KDRTV.COM, TWITTER, FACEBOOK, INSTAGRAM na kwenye YOU TUBE.
Mbali na hayo, MIJOGE JR. ni Mwigizaji na hupenda kukuza usanii.

Where Do Our Friends Go When We Need Them?

Reconcile For the Sake of Unity in Kenya. Church Leaders Urge President Uhuru and Opposition Chief Raila