in , ,

Nitagonga Kichwa Chake Kalonzo Kwa Bibilia Iwapo Hataapishwa- Johnson Muthama

Aliyekuwa seneta wa Machakos Johnson Muthama amehapa kugonga Kalonzo Musyoka kwa bibilia iwapo hataapishwa
Aliyekuwa seneta wa Machakos Johnson Muthama amehapa kugonga Kalonzo Musyoka kwa bibilia iwapo hataapishwa

-Aliyekuwa seneta wa Machakos Johnson Muthama amehapa kugonga Kalonzo Musyoka kwa bibilia iwapo hataapishwa

-Muthama alitoa tamko hilo alipohudhuria mazishi kule Kaunti ya Kitui

-Hapo awali Kalonzo alisema kwamba ako tayari kuapishwa kama naibu wa Raila Odinga baada ya kukosa hafla ya kuapishwa kwake Raila mnamo January 30.

Aliyekuwa seneta wa Machakos Johnson Muthama, amemtahadharisha kiongozi wa Wiper na naibu wa kinara wa muungano wa NASA Kalonzo Musyoka kwamba atamgonga kwa bibilia iwapo hataapishwa kama naibu wa rais wa wanchi

“Nahapa mbele ya Mwenyezi Mungu, Kama Kalonzo hataapishwa, nitamgonga kwa kichwa kwa bibilia,” alihapa Muthama

Muthama alisema hayo alipokuwa akihutubia watu kwenye mazishi kule kaunti ya Kitui aliporejelea ripoti kwamba Kalonzo alifungiwa ndani ya nyumba siku ambayo angefaa kuapisha pamoja na Raila Odinga.

180130131153-01-raila-odinga-0130-exlarge-169-300x168 Nitagonga Kichwa Chake Kalonzo Kwa Bibilia Iwapo Hataapishwa- Johnson Muthama
Raila Odinga akila kiapo kuwa rais wa wananchi mnamo Januari 30, 2017 katika bustani la Uhuru Park

Kulingana na ripoti za hapo awali, Johnson Muthama alifichua kwamba, pia yeye alifungiwa ndani alipoenda kumchukua Kalonzo ili waelekee kwenye bustani la Uhuru Park alikotarajiwa kula kiapo.

Msemo wa Johnson Muthama umejiri kipindi kifupi baada ya Kalonzo kupuuzilia mbali madai kwamba aliratibiwa kuapishwa Jumanne, Februari 28.

Ikumbukwe kwamba, hapo awali, Kalonzo alisemwa kwamba ako tayari kuapishwa kama naibu wa rais wa wanchi, wazo ambalo alidai kwamba vigogo wa muungano wa NASA baado wanalijadili.

kalon Nitagonga Kichwa Chake Kalonzo Kwa Bibilia Iwapo Hataapishwa- Johnson Muthama
Kalonzo alisema kwamba vigogo wa NASA baado wanajadili mpango wake wa kuapishwa

Hata hivyo, naibu wa kiongozi wa Wiper Farah Maalim alitoa wazo kinzani huku akisema kwamba Kalonzo hataapishwa tofauti na ilivyoratibiwa hapo awali.

Pai, alidai kwamba swala la kula kiapo ilikuwa ni wazo lake Raila na wala vigogo wengine hawakua wameunga mkono kamilifu wazo hilo.

Kulingana na ripoti za awali za KDRTV.com, tulieleza kwamba kulingana Kalonzo, hafla ya kuapishwa kwake Raila ilikuwa kinyume cha katiba na walidhani angekamatwa.

Kalonzo alihoji kwamba, vigogo wa NASA walikubaliana Raila ale kiapo pekee yake ndipo akitiwa nguvuni, vinara wengine wabuni taratibu za kumpigania aachiliwe huru.

Hata hivyo, aligundua kwamba, serikali haingeweza kumkamata Raila kwa kuogopa kuzuka kwa machafuko ya kisiasa nchini.

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Loading…

Drop a Comment Below

Written by RASHID EMI

RASHID EMI (+254 763 789 784) ni Mtangazaji na Mwandishi wa habari kutoka KENYA na huripoti matukio yote ya ndani na nje ya KENYA kila siku kupitia KDRTV.COM, TWITTER, FACEBOOK, INSTAGRAM na kwenye YOU TUBE.
Mbali na hayo, RASHID EMI. ni Mwigizaji na hupenda kukuza usanii.

Wakazi wa Lamu wamepuzilia mbali sherehe za siku ya wapendanao wakihoja kwamba wao wanapendana kila siku

MAKALA YA SIKU YA WAPENDANAO: Wakazi Wa Lamu Wapuuzilia Mbali Sherehe Za Siku Ya Wapendanao (Valentines Day)

Bunge la kitaifa limeidhinisha watu 9 waliopendekezwa na Rais Kenyatta kuhudumu katika baraza la mawaziri

Bunge la Kitaifa Limeidhinisha Watu 9 Waliotueliwa Kuhudumu Katika Baraza La Mawaziri