in , ,

Jaji David Maraga ni Kibaraka Cha NASA- Viongozi wa Milma Kenya

Je Viongozi Kutoka Mlima Kenya Watamuunga Mkono William Ruto 2022?

Jaji David Maraga ni kibaraka cha NASA wasema viongozi wa Milma Kenya
Jaji David Maraga ni Kibaraka Cha NASA- Viongozi wa Milma Kenya

-Viongozi kutoka mlima Kenya wameshtumu jaji mkuu David Maraga kwa kupendelea upande wa muungano wa upinzani NASA.

-Kundi hilo la wabunge kutoka mlima Kenya pia wamepigia debe ushirikiano miongoni mwao ili kuweza kuwa na usemi mkubwa wakati Rais Uhuru atakuwa amehitimisha awamu yake ya uongozi

-Pia wameelezea nia yao ya kumuunga mkono naibu rais wiliam Ruto ifikapo mwaka wa 2022 na kuhapa kutomwunga mkono Gideon Moi.

Kundi moja la wabunge kutoka majimbo ya Laikipia, Kirinyaga, Nyandurua na Nakuru, wamemshtumu jaji mkuu David Maraga kwa kuegemea upande wa muungano wa upinzani NASA kwa kuwa idara ya mahakama imekuwa ikifanya maamuzi yanayopendelea upinzani

HABARI NYINGINE:Mawakili Kuanda Mgomo wa Kitaifa, Wanasuta  Serikali Kudharau Idara Ya Mahakama

Wamehoji kwamba ingawa kila mmoja ana jukumu la kulinda sheria, matukio ya hivi majuzi nchini ni wazi kwamba idara ya mahakama inaegemea upande wa upinzanzi.

“Jaji Maraga awache kuruhusu watu wa NASA kutumia koti, kila siku wanaapisha halafu wanakimbia kwa koti, wanalipa shilingi hamsini halafu huyu Maraga anawambia waende nyumbani,”alisaili mmoja wa wabunge hao.

Wabunge hao wakiongozwa na mbunge wa Kinangop pia wamechukua nafasi hiyo kupigia debe ushirikiano miongoni mwao ili kuhakikisha kwamba watakuwa na usemi mkubwa katika serikali ya naibu rais William Ruto iwapo atapita.

Aidha, wabunge hao wa mlima Kenya wameshtumu nia ya kuunga mkono Gideon Moi katika uchaguzi wa mwaka 2022 huku wakihoji kwamba, hakuna sheria inyoonyesha kuwa rais lazima awe mtoto wa rais.

Hatua hii ya wabunge hao imejiri siku chahce baada ya jaji mkuu David Maraga kushtumu hatua ya serikali kuu kuweza kukaidi agizo la mahakama kuhusu maswala muhimu nchini haswa wakati huu kunaposhuhudiwa joto kali la kisiasa.

Mahakama iliamuru mamlaka ya mawasiliano nchini kufungua mitambo ya runinga za Citizen, KTN, NTV na Inooro baada ya kuzimwa mnamo Januari 30 kuhusiana na hafla ya kuapishwa kwa Raila Odinga, hata hivyo serikali ilikaidi agizo hilo na kuendelea kuzima runinga hizo.

Kwa upande mwingine, agizo la mahakama ya kutaka Miguna Miguna achiliwe huru na badala yake kupewa dhmamani pia ilikiukwa na serikali. Tukio jingine in pale Mahakama kuu ilipoamuru maafisa wakuu wa polisi kuwasilishwa Miguna Miguna mahakamani wakiwa wameandamana naye lakini hilo agizo pia lilikiukwa.

PIA SOMA:Watu 9 Waliopendekezwa Kuwa Mawaziri Kujua Hatima Yao Jumatano Lijalo, Rafael Tuju Hatahojiwa

Sasa chama cha mawakili LSK imetangaza mgomo wa kitaifa utakaodumu kwa muda wa siku tano kuanzia kesho Februari 12, mgomo huo unalengwa kulalamikia hatua ya serikali kuu kudharau idara ya mahakama.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Loading…

Drop a Comment Below

Written by RASHID EMI

RASHID EMI ni Mtangazaji na Mwandishi wa habari kutoka KENYA na huripoti matukio yote ya ndani na nje ya KENYA kila siku kupitia KDRTV.COM, TWITTER, FACEBOOK, INSTAGRAM na kwenye YOU TUBE.
Mbali na hayo, MIJOGE JR. ni Mwigizaji na hupenda kukuza usanii.

Foreign Envoys Piles Pressure on Raila Odinga to Recognize and Respect Uhuru as President as Avenue for Dialogue

LATEST: Raila Rebukes Foreign Envoys for Pressuring him to Recognize Uhuru as President