in ,

HUZUNI NA MAJONZI: Hafla Ya Kuwaaga Wahasiriwa wa Ajali Ya Ndege ya Ziwa Nakuru Ilifanyika Leo

Wakazi wa Nakuru walianda hafla ya kuwaaga na kuzifariji familia za wahasiriwa wa ajali ya ndege ya Ziwa Nakuru
Wakazi wa Nakuru walianda hafla ya kuwaaga na kuzifariji familia za wahasiriwa wa ajali ya ndege ya Ziwa Nakuru

Wakazi wa Nakuru walianda hafla ya kuwaaga na kuzifariji familia za wahasiriwa wa ajali ya ndege ya Ziwa Nakuru ambao miili yao haijapatikana

-Wingu la simanzi lilitanda kwenye hafla hiyo huku watu na wanasiasa wakiwapa heshima za mwisho wahasiriwa wa ajali hiyo

Hafla ya kuwaaga na kufariji familia za wahasiriwa wawili wa ajali ya ndege ya Ziwa Nakuru ilifanyika leo Jumamosi, Februari 10 katika mbuga ya wanyama ya kitaifa ya Nakuru.

HABARI NYINGINE:Raila Kuanza Kufanya Kazi Kama Rais, Ako Tayari Kumenyana Na Jubilee

Hata hivyo, miili ya wahasiriwa wawili ambao ni John Mapozi na Sam Gitau haijapatikana baado tangu kutokea ajali hiyo. Aidha, miili ya rubani Apolo Malowa, Anthony Kipyegon na Veronica Muthoni ilipatikana.

Sam Gitau na John Mapozi walikuwa wameajiriwa na Susan Kihiga ambaye aliwamiminia sifa vijana hao kama waliokuwa wakamavu.

Jumbe za Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto zilisomwa na mkurugenzi ya mawasiliano ya mtandao katika Ikulu Denis Itumbi, huku Rais na naibu wake wakiahidi kutenga nafasi kujumuika na familia hizo

Idadi kubwa ya watu pamoja na wanasiasa walihudhuria hafla hiyo huku wingu la simanzi likishamiri mazingira hayo.

Wanasiasa wakiongozwa na seneta wa kaunti ya Nakuru Susan Kihiga pamoja na wabunge kama vile Davida Gikaria na Liza Chelule ni miongoni mwa waheshimiwa waliohudhuria sherehe hiyo.

“Ni bahati mbaya hatutawaona marafiki zetu tena. Imekuwa vigumu kwetu kufikia maamuzi. Tunamwomba Mwenyezi Mungu kuzifariji familia hizo tano na azipe nguvu,”alisema Kihiga.

Mamake Mapozi Florence Nyambura alihoji kwamba imekuwa miezi matatu ya majonzi huku wakijaribu kufikia maamuzi kwamba hawatazipata maiti za wapendwa wao.

“Ni bahati mbaya maiti ya mvulana wetu mpendwa haiwezi kupatikana. Tumaini zetu za kumpata zimegeuka hangaiko. Hata hivyo, baado tunamwomba Myenyezi Mungu atupe faraja katika kipindi hiki kigumu,” shangazi wa Gitau Elizabeth Njeri alisema hapo awali kwenye mahojiano

Hadi sasa, ni boti moja tu ndiyo imekuwa ikipiga doria katika Ziwa Nakuru kwa juhudi za kutafuta miili hiyo mingine baada ya ajali hiyo kufanyika Oktoba 21 mwaka jana.

PIA SOMA:NAJUA UHURU ANANIANDAMA LAKINI NIKO TAYARI KUKABILIANA NAYE- RAILA ODINGA

Serikali kuu, serikali ya kaunti, kamati ya kitaifa ya majanga na mikasa, wanajeshi wa maji, idara ya polisi, polisi wa kulinda wanyamapori na wapiga mbizi kutoka Ziwa Nakuru walihusika katika juhudi za kutafuta maiti za wahasiriwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Loading…

Drop a Comment Below

Written by RASHID EMI

RASHID EMI (+254 763 789 784) ni Mtangazaji na Mwandishi wa habari kutoka KENYA na huripoti matukio yote ya ndani na nje ya KENYA kila siku kupitia KDRTV.COM, TWITTER, FACEBOOK, INSTAGRAM na kwenye YOU TUBE.
Mbali na hayo, RASHID EMI. ni Mwigizaji na hupenda kukuza usanii.

NASA Chief Raila Odinga Accuses Jubilee Government of Violating the  Constitution and Human Rights

Watu 9 Waliopendekezwa Kuwa Mawaziri Kujua Hatima Yao Jumatona Lijalo, Rafael Tuju Hatahojiwa

Watu 9 Waliopendekezwa Kuwa Mawaziri Kujua Hatima Yao Jumatano Lijalo, Rafael Tuju Hatahojiwa