in , ,

MAKUBWA: WAKILI WA MIGUNA MIGUNA AKAMATWA NA POLISI NAIROBI!

Polisi mnamo Jumapili, Februari 11 usiku walimtia nguvu wakili Harun Ndubi kwa kuendesha gari akiwa mlevi
Polisi mnamo Jumapili, Februari 11 usiku walimtia nguvu wakili Harun Ndubi kwa kuendesha gari akiwa mlevi

-Polisi mnamo Jumapili, Februari 11 usiku walimtia nguvu wakili Harun Ndubi kwa kuendesha gari akiwa mlevi

-Polisi walisema kwamba Ndubi alikamtwa karibu na lango D linaloelekea Ikulu ambako gari lake lilipatikana likiwa limeegeshwa

-Ndubi alilawama kwamba alivurutwa na watu wasiojulikana na kutiwa nguvuni badala ya kupelekwa hospitali

-Ndubi ni miongoni mwa mawikili waliomwakilisha Miguna Miguna mahakamani baada ya kustakiwa kwa kushiriki katika hafla ya kula kiapo kwa Raila Odinga

Wakili wa haki za kibinadamu, Harun Ndubi alikamatwa mnamo Jumapili, Februari 11 usiku na kupelekwa korokoroni akishtumiwa na kosa la kuendesha gari akiwa mlevi

HABARI NYINGINE:HABARI ZA HIVI PUNDE: Mawakili Wafutilia Mbali Mgomo Wao, Wanihitaji Muda Zaidi Kijiandaa

Polisi walieleza kwamba, wakili huyo alikamatwa karibu na Lango D linaloelekea katika Ikulu ambako gari lake lilipatikana limeegeshwa kwenye barabara ya Jakaya Kikwete.

Kulingana na taarifa za Daily Nation, wakili na mwanaharakati za haki za kibinadamu huyo aliripoti kwamba, alivurutwa na kutiwa nguvuni akiwa katika hali mahututi.

Mkuu wa polisi Nairobi Japheth Koome alisema kuwa wakili huyo atashtakiwa kwa kosa la kuendesha gari akiwa mlevi.

Inasemekana kwamba Ndubi alikuwa akielekea nyumbani wakati alipolemewa na alichokila ndipo alipoamua kusimamisha gari eneo lile

Baadaye alipelekwa hadi kwenye kituo cha polisi cha Kileleshwa na kufungiwa huku akingojea kushtakiwa.Jitahada za kuweza kumtoa kwa dhamana ziligonga mwamba huku maafisa wa polisi kwenye kituo hicho wakieleza kwamba, walipata amri kwamba waenedelea kumweka korokoroni.

Wakili Harun Ndubi alikuwa miongoni mwa wale mawakili waliomwakilisha jenerali wa vuguvugu la NRM Miguna Miguna baada ya kustakiwa na serikali kwa kuhusika katika hafla ya kula kiapo kwake Raila Odinga.

PIA SOMA:Jaji David Maraga ni Kibaraka Cha NASA- Viongozi wa Milma Kenya

Miguna Miguna baadaye alifurushwa nchini na kusafirishwa hadi nchini Canada ambako pia ana uraia. Hii ilikuwa ni baada ya inspekta jenerali wa polisi Joseph Boinett na mkurugunzi wa idara ya upelelezi George Kinoti kukaidi agizo la mahakama lililowataka kufika mahakamni wakiwa wameandamana na Miguna Miguna. Hapo awali pia, mahakama iliamuru Miguna Miguna Kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi 50,000 lakini, serikali pia ilikaidi agizo hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Loading…

Drop a Comment Below

Written by RASHID EMI

RASHID EMI ni Mtangazaji na Mwandishi wa habari kutoka KENYA na huripoti matukio yote ya ndani na nje ya KENYA kila siku kupitia KDRTV.COM, TWITTER, FACEBOOK, INSTAGRAM na kwenye YOU TUBE.
Mbali na hayo, MIJOGE JR. ni Mwigizaji na hupenda kukuza usanii.

Mawakili nchini Kenya kupitia chama cha wanasheria nchini LSK wameahairisha mgomo wao kutenga muda Zaidi kwa maandalizi thabiti

HABARI ZA HIVI PUNDE: Mawakili Wafutilia Mbali Mgomo Wao, Wanihitaji Muda Zaidi Kijiandaa

Petition Challenging Ojaamong’s Victory Dismissed as Petitioner Directed to Pay Ksh. 12 Million Cost