in

EU yasema haina nia ya kutatiza uchaguzi mkuu nchini


Na Mate Tongola
NAIROBI, KENYA, Umoja wa mataifa ya bara Uropa umesema kuwa hauna nia yoyote ya kutatiza au kuhitilafiana na uchaguzi mkuu ujao humu nchini bali nia na lengo kuu ni kuhakikisha uchaguzi huo ni wa huru na haki.
Akizungumza katika ofisi za Tume ya Uchaguzi, IEBC mjini Kisumu, Kiongozi wa Umoja huo ukanda wa Afrika Mashariki Bruno Pozzi amesema kuwa tayari wametenga fedha za kufanikisha shughuli ya uchaguzi huo wa Agosti 8.
Ikumbukwe kuwa wakati wa sherehe za siku kuu ya Jamhuri mwaka uliopita, Rais Uhuru Kenyatta alikwaza utendakazi wa baadhi ya mashirika ya kijamii yanayopokea ufadhili kutoka ng’ambo akisema kuwa yanatumiwa kutatiza uchaguzi mkuu ujao.

 

Kenya set to form convention bureau to boost business tourism

Kitui police hunt down suspected Somali bandits