in , ,

Bunge la Kitaifa Limeidhinisha Watu 9 Waliotueliwa Kuhudumu Katika Baraza La Mawaziri

Bunge la kitaifa limeidhinisha watu 9 waliopendekezwa na Rais Kenyatta kuhudumu katika baraza la mawaziri
Bunge la kitaifa limeidhinisha watu 9 waliopendekezwa na Rais Kenyatta kuhudumu katika baraza la mawaziri

-Bunge la kitaifa limeidhinisha watu 9 waliopendekezwa na Rais Kenyatta kuhudumu katika baraza la mawaziri

-Wabunge wa muungano wa upinzani walisusia kikao hicho kwa kuondoka bungeni punde tu mjadala kuhusu ripoti hiyo ya kamati ya bunge ulipoanza kujadiliwa.

-Hapo jana rais Uhuru Kenyatta aliongoza mkutano wa chama cha Jubilee huku akirai wabunge wa Jubilee kuhakikishwa kwamba ripoti kuhusu watu tisa aliowapendekeza imepitishwa.

Bunge la kitaifa hivi leo Jumatano, Februari 14 liliidhinisha ripoti ya kamati ya uteuzi ya bunge iliyopata watu tisa waliopendekezwa kuwa mawaziri kutokuwa na doa lolote. Wabunge wa Jubilee waliunga mkono kwa kauli moja ripoti hiyo huku mara nyingine wenzao wa muungano wa upinzani wakisusia kikao hicho.

HABARI NYINGINE:Nitagonga Kichwa Chake Kalonzo Kwa Bibilia Iwapo Hataapishwa- Johnson Muthama

Wabunge wa muungano wa upinzani walitoka bungeni pindi tu mjadala kuhusu ripoti hiyo ya kamati ya uteuzi ya bunge ilopoanza kujadiliwa. Hatua hii iliwapelekea wenzao wa Jubilee kuwashtumu vikali.

Mawaziri Magret Kobia (Utumishi wa Umma), Keriako Tobiko (Mazingira), Farida Karoney (Ardhi), Ukur Yattani (Leba), Peter Munya (Jumia ya Afrika Mashariki), John Munyes (Madini), Simon Chelugui (Maji) na Rashid Mohammed Achesa (Michezo na Utamaduni) sasa wangojea tu kuapishwa rasmi.

Hata hivyo, kuidhinishwa kwake Rashid Mohammed Achesa kama waziri wa Michezo na Utamaduni ilizua tumbo joto miongoni mwa baadhi ya wabunge huku wakitilia shaka kiwango chake cha elimu. Lakini, Bwana Achesa alipata afueni baada ya wabunge wa Jubilee wakiongozwa na Aden Duale kumuunga mkono na kusema kwamba, Achesa atawakilisha watu maskini na vijana katika nchi ya Kenya.

ras-1 Bunge la Kitaifa Limeidhinisha Watu 9 Waliotueliwa Kuhudumu Katika Baraza La Mawaziri
Uteuzi wa waziri wa michezo na Utamaduni Rashid Mohammed Achesa ilipingwa vikali na baadhi ya wabunge wakitilia shaka kiwango chake cha elimu

Duale alihoji kwamba sio lazima mtu ahitimu kutoka chuo kikuu cha kifahari ndiposa apewa cheo. Wabunge hao sasa wamemshauri Bwana Achesa kuendelea na masomo huku akihudumu kama waziri vile vile.

PIA SOMA:MAKALA YA SIKU YA WAPENDANAO: Wakazi Wa Lamu Wapuuzilia Mbali Sherehe Za Siku Ya Wapendanao (Valentines Day)

Wabunge wa Jubilee pia wamsihi spika wa bunge la kitaifa Justin Muturi kashuari wabunge wa muungano wa upinzani kufichua orodha yao ya baraza la la mawaziri ili kubaini msimamo wao.

Kikubwa zaidi sasa, ni bunge hilo kuwapiga msasa walioteuliwa kuwa makatibu katika wizara mbali mbali na vile vile waliopendekezwa na rais Kenyatta kuwa mabalozi.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Loading…

Drop a Comment Below

Written by RASHID EMI

RASHID EMI (+254 763 789 784) ni Mtangazaji na Mwandishi wa habari kutoka KENYA na huripoti matukio yote ya ndani na nje ya KENYA kila siku kupitia KDRTV.COM, TWITTER, FACEBOOK, INSTAGRAM na kwenye YOU TUBE.
Mbali na hayo, RASHID EMI. ni Mwigizaji na hupenda kukuza usanii.

Aliyekuwa seneta wa Machakos Johnson Muthama amehapa kugonga Kalonzo Musyoka kwa bibilia iwapo hataapishwa

Nitagonga Kichwa Chake Kalonzo Kwa Bibilia Iwapo Hataapishwa- Johnson Muthama

NASA Legislators Walk Out of a Sitting Amid Cabinet Nominees Approval