in , ,

Watu 9 Waliopendekezwa Kuwa Mawaziri Kujua Hatima Yao Jumatano Lijalo, Rafael Tuju Hatahojiwa

Watu 9 Waliopendekezwa Kuwa Mawaziri Kujua Hatima Yao Jumatona Lijalo, Rafael Tuju Hatahojiwa
Watu 9 Waliopendekezwa Kuwa Mawaziri Kujua Hatima Yao Jumatona Lijalo, Rafael Tuju Hatahojiwa

-Watu 9 waliopendekezwa na rais Uhuru Kenyatta kuhudumu katika baraza la mawaziri watabaini hatima yao Jumatano, Februari 14

-Kamati ya uteuzi ya bunge sasa imeanza kuanda ripoti yake baada ya kukamilika kwa zoezi la kuwapiga msasa watu tisa waliopendekezwa kuwa mawaziri

-Hata hivyo, imebainika wazi kwamba Rafael Tuju ambaye hakupewa wizara yoyote sasa hatahojiwa na kamati hiyo ya uteuzi ya bunge

Watu 9 waliopendekeza na Rais Uhuru Kenyatta kuhudumu katika baraza la mawaziri watajua hatima yao siku ya Jumatano Juma lijalo baada ya zoezi la kuwapiga msasa kukamilika

HABARI NYINGINE:HUZUNI NA MAJONZI: Hafla Ya Kuwaaga Wahasiriwa wa Ajali Ya Ndege ya Ziwa Nakuru Ilifanyika Leo

Kamati ya uteuzi ya bunge sasa imeanza kuanda ripoti yake baada ya zoezi la kuwapiga msasa walioteuliwa na Rais Uhuru kuwa mawaziri kukamilika.

Kulingana na spika wa bunge la kitaifa Justin Muturi, ripoti hiyo inafaa kuwasilishwa bungeni kujadiliwa Jumanne na kuamuliwa Jumatano. Muturi ameeleza kwamba anayo imani kwamba kufikia Jumatano, zoezi la uteuzi wa waliopendekezwa kuwa mawaziri litakuwa limekamilika jinsi katiba inavyohitaji

Wakati huo huo, ni wazi sasa kwamba Rafael Tuju ambaye hakupewa wizara yoyote hatahojiwa na kamati ya uteuzi ya bunge kama walivyofanyiwa wenzake. Hii ni kwasababu Tuju atakuwa akihudhuria baadhi ya vikao vya baraza la mawaziri na kufanya kazi anapohitajika.

Jukumu la Rafeal Tuju katika baraza la mawaziri ni kuhakikisha kwamba baraza hilo linatekeleza majukumu yake kulingana na manifesto ya chama cha Jubilee, vile vile ataendelea kuhudumu kama katibu mkuu wa chama cha Jubilee

Ripoti hiyo ya uteuzi yaweza kupitishwa na bunge au bunge linawezaamua kuifanyia marekebisho. Lakini hali ilivyo ni kwamba, asilimia ya ripoti hiyo kupitshwa iko juu ikizingatiwa idadi kubwa ya wabunge wa Jubilee bungeni

PIA SOMA:George Kinoti na Joseph Boinett Warushia Mzigo Idara Ya Uhamiaji Kuhusu Kufurushwa Kwa Miguna Miguna

Sasa spika wa bunge la kitaifa Muturi anahitajika kuwasilisha bungeni majina ya watu waliopendekezwa kuwa mabalozi Jumatano lijalo ili kamati husika za bunge zianze kuwahoji watu hao.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Loading…

Drop a Comment Below

Written by RASHID EMI

RASHID EMI (+254 763 789 784) ni Mtangazaji na Mwandishi wa habari kutoka KENYA na huripoti matukio yote ya ndani na nje ya KENYA kila siku kupitia KDRTV.COM, TWITTER, FACEBOOK, INSTAGRAM na kwenye YOU TUBE.
Mbali na hayo, RASHID EMI. ni Mwigizaji na hupenda kukuza usanii.

Wakazi wa Nakuru walianda hafla ya kuwaaga na kuzifariji familia za wahasiriwa wa ajali ya ndege ya Ziwa Nakuru

HUZUNI NA MAJONZI: Hafla Ya Kuwaaga Wahasiriwa wa Ajali Ya Ndege ya Ziwa Nakuru Ilifanyika Leo

Wahudumu Katika Sekta ya Usafiri Kiambu Wanataka Charity Ngilu Akamatwe Kwa Kuamuru Magari Yachomwe

Wahudumu Katika Sekta ya Usafiri Kiambu Wanataka Charity Ngilu Akamatwe Kwa Kuamuru Magari Yachomwe